Sport | Kanu Nwankwo atangaza kuwania Uraisi wa Nigeria 2019
Aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, Kanu Nwankwo alifunguka katika maojiano na Goal.com na kuonesha nia ya kuwania uraisi Nigeria, baada ya kile kilichotokea kwa George Weah ambaye kwasasa ni Raisi wa Liberia.
Hatimaye mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, kanu ametangaza kuwa atawania kuwa Raisi wa Nigeria mwaka 2019.
Kanu ambaye alichezea Ajax, Inter Milan na Arsenal, alisema alikuwa na ndoto ya kubadili taswira ya maendeleo kwenye nchi yake ya nigeria husasani uchumi na usalama.
Mshindi wa Ligi ya Mabingwa mwaka 1995, hakuficha upendo wake na nia ya kuwa mwanasiasa baada ya kustafu mwaka 2012 huko Postmouth.
Kabla ya kutangaza kuwania uraisi mwaka 2019, mchezaji bora wa Afrika 1996 na 1999, alizungumza kwanza na wafuasi wake kadhaa au watu wake wakaribu bila shaka wakamshauri atimize ndoto yake ya kuendeleza nchi yake.
Post a Comment