MISHE-BOY

News | Mtambuwe msanii Emery Joe historia ya maisha yake kimuziki na aliyoyapitia

Tambuwa ukitaka kujua ku shine hapa Burundi ni juhudi zako mwenyewe kwa kupiga kazi bila kulala na mwisho wa siku ninaimani utafikia malengo yako.

Anaitwa Emery Ntakarutimana akifahamika sana kwajina la Emery Joe ni raia wa Burundi, alizaliwa Mkoani Gitega mwaka 1990,. 

Mwaka 2007 alifanikisha kupata elimu ya msingi Kanyosha I iliyopo kanyosha mjini Bujumbura, aliendelea na elimu ya Sekondari na kuhitimu mwaka 2014 katika shule ya Lycée de la Convivialité iliyopo kanyosha, akisomea lettres Modernes.
Emery Joe aliendeleza elimu ya cho kikuu nchini Kenya akisomea Business World hadi mwaka 2017.

Mwaka 2004-2007 Alionekana kupenda muziki sana na kuanza kama densa katika kundi itwayo Yvant Muzika (Boys 2 Man) uko Centre Jeune Kamenge, hata hivyo alianza kukrem nyimbo za wasanii waliokuwa wa kihit kipindi kile nchini na nje ya nchi.

Mwaka 2008, alianza kutunga mwenyewe nyimbo polepole na kufanikisha kuingia studio kwa mara ya kwanza na kurikodi wimbo wake uitwao kirezi.  hali iliendelea kuwa ngumu kwake kwa kupenda  shule na muziki ila hakukata tamaa aliendelea na kwasasa ana nyimbo nane (8) huku anatarajia kuachia hivi karibuni wimbo wake mpya uitwao Vyose ni Mumutwe.

Ebu jaribu kutazama moja ya kazi yake hapa:

Hakuna maoni