Sport | UEFA yatangaza mabadiliko katika Ligi ya Mabingwa Msimu ujao
UEFA imefanya mabadiliko zaidi katika sheria zake zinazoongoza Ligi ya Mabingwa na Europa League, kuanzia msimu ujao, itawawezesha timu kusajili wachezaji watatu wapya waliohamishwa wakati wa majira ya baridi na tayari wamecheza michezo ya Ulaya ( Champions League na Europa League).
Kuanzia sasa timu zinazo shiriki katika Ligi ya Mabingwa zinapashwa kugawa Euro Bilioni 3,4 badala ya Euro Bilioni 2,3 wakati wanaoshiriki Europa League watagawa kwa jumla Euro Milioni 500 badala ya € 400 milioni ya leo.
Kuanzia msimu ujao timu zitasajili wachezaji watatu kwenye hatua ya makundi - katika ligi ya Mabingwa sawa na Europa ligi hata hatua ya mwisho. Hata kama wachezaji hawo watakua tayari wamecheza mashindano na timu zao ya zamani, kama ilivyokuwa kesi ya Philip Coutinho ambaye hakuweza kucheza Ligi ya Mabingwa na Barca baada ya kushiriki katika hatua ya makundi na Liverpool au kama Aubameyang alipojiunga na Arsenal kutokea Dortmund.
Pia mabadiliko mengine UEFA ilibadili ni,
- kocha watakuwa na uwezo ya kutumia mabadiliko ya nne wakati wa ziada ( Prolongations).
- Wachezaji 23 waruhusiwa kuingia kwenye orodha ya mechi (feuille de match) badala ya 18 ya leo.
- Na klabu iliyoshinda Europa Ligi ( Kombe la UEFA) mara tatu kwa mfululizo au mara tano katika historia yake, lazma timu hiyo kuvaa jezi ikiwa na alama tofauti.
Post a Comment