Sport [ Faouzi Benzarti ndie Kocha mpya wa WAC Cassablanca
Wiki baada ya kufukuzwa kwa kocha Houcine Ammouta, WAC Casablanca imechukua kocha mpya.
Faouzi Benzarti, ambaye ameamua kuacha nafasi yake katiaka klabu ya Esperance Tunis
mwishoni mwa Desemba, licha ya kuchukua kombe la heshima cha ubingwa wa automn.
Faouzi 67, raia wa Tunisia anarudi nchini Moroko, miaka minne baada ya ziara yake na Raja Casablanca.
Mshindi
wa Ligi ya Mabingwa mwaka 1994 akiwa kama kocha wa Esperance, Faouzi Benzarti
amesaini mkataba kwa muda wa mwaka moja na nusu na atakuwa na lengo la
kuhifadhi ubingwa ambao klabu hiyo ilishinda mwaka jana na Wydad .
Post a Comment