MISHE-BOY

MISHE MISHE NEWZ | Nyota njema huonekana asubuhi, asema Gaga Blue


Msanii wa kizazi kipya kutoka Burundi, Gaga Blue ambae kwasasa anazidi kutamba na kibao chake Ivo Ivo aliyomshirikisha msanii kutoka Tanzania, Young D. kwasasa anendelea na kazi ya muziki nchini tanzania katika arakati ya kutengeneza muziki wake kimataifa zaidi.

Siku za nyuma msanii huyu aliwai kusema kwamba yeye ndie msanii wakuiga kutoka Burundi, kwasasa amezua nyingine na kusema kwamba nyota yake inazidi kungaa na kuonekana kinara wa Burundi fleva.

Msanii huyo kupitia kipindi cha Morning Trumpet ya mtangazaji Sophia Kilumanga kwenye Azam Tv, alitamka maneno aya :
'' Ninacho pata bahati ya kutangaza kazi zangu nje ya nchi kama nchi hii ina ma staa kibao wa Afrika mashariki, bila shaka fursa hii siwezi kuichezea na kama ninavyo sema kila siku  kama mimi ni msanii wa kuiga basi nitahakikisha kauli hii iwe kweli''. Alisema gaga Blue.
Msanii huyo ambae kwasasa anaonekana kama msanii anaejituma sana kweli swala la muziki, amesema kuwa jinsi kazi zake zinazidi kupendwa na kupitishwa nje ya nchi humpa faradja sana na moyo wa kujituma zaidi.

Hakuna maoni