MISHE MISHE Newz | Msanii Gaga Blue asema kwamba yeye ndie msanii wa kuigwa kwenye Burundi Fleva
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambae anafanya vizuri kwa sasa Gaaga Blue,
amesema kwamba yeye kama kwenda nje (Tanzania) au kufanya vipindi ni
kwasababu ana plan ya muziki na kuitambulisha muziki wake kimataifa.
Gaga Blue amesema kwamba lazima afanye mambo makubwa nchini hapo ambazo
zitatengeneza uthamani kwa wasanii wa Burundi kwa kulipwa pesa kubwa na
pia mataifa itambue kama Burundi kuna vipaji vya hali ya juu.
Aidha
ameonyesha kushangazwa na baadhi ya wasanii ambao wanajishushia thamani zao kwa kufanya kazi ya muziki bila plan, na kuongeza kusema kwamba yeye (Gaga) ndie ndie msanii wa kuigwa kutoka Burundi na lazima mashabiki wa Burundi Fleva watajivunia jina yake kwenye ulimwengu wa muziki.
(Picha ni Gaga Blue kutoka Burundi na Sheta wa Bongo wakimaliza kufanya kipindi cha Lil Ommy wa Times FM, Tanzania).
(Picha ni Gaga Blue kutoka Burundi na Sheta wa Bongo wakimaliza kufanya kipindi cha Lil Ommy wa Times FM, Tanzania).
Post a Comment