DIDIER KAVUMBAGU KUWEKA RIKODI YANGA
ni mchezaji mrundi ambae amewahi kuichezea klabu nyingi hapa nchini Burundi kwajina lake alisi ni DIDIER Kavumbagu , Kikosi
cha Yanga, leo Alhamisi kinaanza safari ya kurudi nchini kikitokea
kambini Uturuki, lakini kati ya nyota anayerudi kishujaa ni Mrundi huyo,
aliyeibuka mfungaji bora nchini humo.
tukumbuke kuwa Katika kambi hiyo ya Yanga, ambayo ilikuwa katika
mji wa Antalya, kikosi hicho kilicheza michezo minne ya kirafiki na
klabu mbalimbali za Ulaya, na kilifunga jumla ya mabao saba na kufungwa
mawili, lakini Kavumbagu akafunga matatu kati ya hayo saba.
na baadhi ya wenye wanamufaham hapa ni Nyota mrefu kuliko wote katika kikosi hicho cha Yanga
alifunga bao la kwanza katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ankara Sekespor,
wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 na mengine yakifungwa na
Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza.
Mshambuliaji huyo aliifungia timu yake tena bao
moja wakati ikicheza dhidi ya Altay S.K ya Uturuki na jingine likifungwa
na Okwi, wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 kabla ya kufanya
hivyo tena katika mchezo wa mwisho wakati timu hiyo ilipotoka sare ya
mabao 2-2 na Simerq PIK ya Azerbaijan na jingine likifungwa na Mrisho
Ngassa.
Kabla ya mchezo huo wa mwisho kikosi hicho
kiliumana na KS Flamurtari ya Albania na kulazimishwa suluhu. Wakati
Kavumbagu akiweka rekodi hiyo alifuatiwa na Okwi raia wa Uganda
aliyefunga mabao mawili huku Kiiza na Ngassa wakifuatia kwa kupachika
bao moja kila mmoja lakini Ngassa akiweka rekodi yake kwa kuwa mzawa
pekee aliyefunga katika ziara hiyo.
Rekodi nyingine ambayo imewekwa na Kavumbagu ni
kwamba nyota huyo amefunga mabao hayo matatu, yote ni mabao ya kwanza ya
Yanga katika kila mchezo akifunga bao la kwanza dakika 10, mchezo wa
pili dakika 46 na wa mwisho dakika 13, na kumfanya kuweka rekodi hiyo
ambayo awali iliwahi kuwekwa na mshambuliaji Jerry Tegete, aliyekuwa
mfungaji bora katika ziara ya timu hiyo katika mji huo msimu uliopita
kwa kupachika mabao mawili.
Post a Comment