MISHE-BOY

Kaze Gilber " Demunga" kapokelewa na mashabiki wapinzani wa Yanga kwenye Uwanja wa Ndege

MASHABIKI wa Yanga jana Jumatano walijazana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumpokea mchezaji wao mpya, Emmanuel Okwi, lakini wakaishia kumpokea beki wa Simba( mrundi), Gilbert Kaze.
j
 watu wameshangaa sana kuona mashabiki wa timu pinzani kumuzunguuka mchezaji Kaze wakati walikua wanakuja kumpokea mchezaji wao wa mpya kutoka uganda,wakiamini Okwi angetua kutoka Uganda, mchezaji huyo hakuonekana na wakiwa wanazidi kusubiri wakakumbana na Kaze majira ya saa 9 alasiri.
tukumbuke kuwa Demunga alikua akitokea Burundi  na akijielekeza zanzibar kwenye kambi ya klabu yake ya simba.
Demunga alipotoka nje ya uwanja alikumbana na mashabiki kibao na waandishi wa habari kiasi cha kumfanya ashituke, lakini baadaye viongozi wa Simba waliofika kumlaki wakamwambia kwamba si yeye anayesubiriwa na umati huo wa Yanga bali ni Okwi.
Lakini, mashabiki wa Yanga wakaanza kumzonga Kaze mpaka kwenye gari wakimpa maneno ya kejeli na kumwambia: “Umepotea njia wewe kwenda Simba...na Okwi anakuja.” Demunga alicheka tu na wala hakujibu chochote. alisema kwa kifupi: “Nashukuru nimerudi salama, kubwa tutakutana uwanjani.” Ndiyo mchezaji pekee aliyekuwa hajajiunga na timu, atakuwa na kazi moja ya kugombania namba na Mkenya Donald Musoti aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia na Joseph Owino raia wa Uganda.
tuwafahamishe kuwa, Demunga
amechelewa kujiunga na wenzake ambao wako chini ya kocha mpya, Zdravko Logarusic kisiwani Zanzibar kwa kile kinachodaiwa, alikuwa anamuuguza mama yake mzazi.
na hao hapa ni ma beki wa 2 vitengemeo wa Simba, ni Owino raia wa Uganda na Kaze Gilbert raia wa Burundi.

Hakuna maoni