MISHE-BOY

makipa wanaolipwa pesa nyingi zaidi ya wenzio duniani

makipa wanaolipwa pesa nyingi, mara nyingi tunazungumuzia tu wachezaji kwa hivi ni Christiano Ronaldo ndiye anaye shikilia nafasi ya kwanza kwa wachezaji kupokea mshahara mkubwa zaidi ya wengine.
kwa makipa :

1. Iker Casillas - Real Madrid

Mambo yake si shwari kwa sasa ndani yaReal Madrid, kutokana na kukaa benchi, lakini jambo hilo halimfanyi kushindwa kuingiza pesa nyingi baada ya mabosi wa timu hiyo kumpatia mkataba mnono.
Mkataba wake ndani ya Real Madrid unamshuhudia Casillas akivuna Pauni 6.3 milioni kwa mwaka na kuwa kipa anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani.

2. Manuel Neuer - Bayern Munich
 
Ni miongoni mwa watu muhimu wanaoifanya Bayern Munich kuwa imara kwa sasa na kuendelea kutesa Ulaya ikiwa pamoja na msimu uliopita kunyakua mataji matatu; Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa Ulaya.Kipa huyo wa kimataifa wa Ujerumani kwa sasa anashika nafasi ya pili kwa kulipwa pesa nyingi baada ya kuvuta Pauni 5.6 milioni kwa mwaka



3. Gianluigi Buffon - Juventus


. Ni kipa aliyedumu kwenye kiwango bora kwa muda mrefu. Kwenye klabu ya Juventus,
Umahiri wake unamfanya kuwa kipa anayeingia mikataba minono inamfanya awemo kwenye orodha ya makipa wanaolipwa pesa nyingi zaidi kwenye mchezo wa soka kwa sasa.

Buffon, ambaye kwa sasa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake ndani ya Juventus ambayo ni bingwa wa Italia, analipwa Pauni 5.5 milioni kwa mwaka.

    4. Petr Cech - Chelsea
 
 
Ni mmoja wa makipa mahiri kabisa katika Ligi Kuu England kwa muongo uliopita. Kwenye klabu ya Chelsea, kipa huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech analipwa Pauni 5.2 milioni kwa mwaka.
 
 
5. Victor Valdes - Barcelona
 
 
Kipa huyo Mhispaniola ambaye hivi karibuni alisema ataihama Barcelona mwishoni mwa msimu pale mkataba wake utakapofika tamati,
 
Valdes yumo kwenye tano bora. Kwa mwaka anavuta Pauni 5 milioni kutokana na mkataba wake wa sasa anaoutumikia Nou Camp. 

Hakuna maoni