Newz | Kingorongoro Apata meneja mpya wa kusimamia kazi zake
Rapa wa muziki kutoka Burundi, Magic Soldier maarufu Kingorongoro ambae kwasasa anatisha industry ya muziki, kupitia track yake iitwayo KASHESHE ambayo amempa shavu Dauphin Dan Color.
Kingorongoro anafanya vyema pia kupitia nyingine iitwayo KIRAKA, Nyota huyu ameamua kumtangaza Manager wake mpya atakayesimamia kazi zake kuanzia sasa na kuachana na Wanda Boy.
Staa huyu wa muziki amepiga hatua nyingine baada ya kufanikiwa kumpata meneja mpya anayejulikana kwa jina la Esteem Young Mash.
"Watu wangu ndoto zangu zimeanza kukamilika, nathibitisha kuwa sasa nimepata meneja ambaye ananijua tangu zamani na fikra zake na zangu kama sare sare tofauti na wale wa awali. Kuna kazi nyingi zinakuja tena nzuri tofauti na miaka za nyuma pamoja na uhamisho wa hapa na pale, nashukuru kwa kuniamini kwa safari hii mpya, twende pamoja sasa", Alisema Kingorongoro mbele ya waandishi wa habari
Post a Comment