MISHE-BOY

Sport | Gabon matatizo yanaendelea, Kocha apatwa na hasira

Baada ya kuchaguliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Gabon  Septemba iliyopita, Daniel Cousin aliamua kumwita mwanasheria wake ili adai wamulipe mshahara wake, bado hajalipwa tangu awasili.

Nchini Gabon licha ya kubadili makocha lakini matatizo yanaendelea, kocha Daniel Cousin anakabiliwa na matatizo ya kutumika bila malipo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini hapo, kocha huyo bado hajapokea hata senti moja tangu achaguliwe kama kocha mkuu wa Gabon.

Ghafla, Cousin alishindwa kuvumilia na akamwita mwanasheria wake ambaye alipeleka barua kwa Waziri wa Michezo wa Gabon, Alain Claude Bilie By Nze.
Mwishowe Waziri alimjibu Cousin kwenye Redio na angalau tunaweza kusema ni kwamba hakufurahia njia ambayo kocha katumia. 

Hata kama kesi hiyi itatatuliwa hivi karibuni, kuna mchezo mkubwa ili Gabon ishiriki kwenye Kombe la Afrika CAN2019 italazimika kushinda mchezo huo dhidi ya Burundi, kwa hiyo Burundi itatumia muda huu kujiandaa vilivyo.


Hakuna maoni