Sport | Kaze Gilbert Demunga wa Universite De Djibouti FC kukaa nje miezi miwili
Beki tegemeo wa timu ya Universite De Djibouti FC ya huko Djiboutie, Kaze Gilbert Demunga aliyesukumwa uwanjani na kuanguka vibaya katika mchezo wa marudio wiki ya pili ya ligi kuu nchini hapo, amefahamika kuvunjika mkono na atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Beki hjuyo aligundulika amevunjika mkono baada ya kupelekwa hospitali mjini hapo baada ya kusukumwa na mshambuliaji katika harakati ya kuokoa mpira katika pambano hilo.
Katika mchezo huo, Universite De Djibouti FC waliibuka na ushindi wa mabao 5-1,
"Baada ya kuona maumivu makali yanaendelea, ndipo uongozi wa timu uliniwahisha hospitali kwa matibabu zaidi na hatimaye daktari kagundua nimepata tatizo kwenye mfupa mdogo wa mkono wa kushoto", alisema beki kaze Gilbert Demunga akiwa amefungwa plasta gumu.
Alisema kwasasa haruhusiwi kufanya lolote hadi baada ya wiki mbili atarudi tena hospitalini hapo ili kuangalia tena kujua mustakabali wake kisoka.
Kwa habari za karibu ya timu Universite De Djibouti FC zimethibitisha kwamba beki wao Demunga atakuwa nje ya uwanja miezi miwili, kwa hiyo ni kama msimu huu kwa beki huyo umekwisha tutarudi kumuona tena msimu ujao.
Post a Comment