MISHE-BOY

Sport | Club Africain yaishutuma TP Mazembe kuwapa sumu

Kuna msemo unatumiwa sana kwenye soka, hasiyekubali kushindwa sio mshindani!
Timu ya Club Africain ilipata kipigo kichafu  ya mabao 8 kwa bila dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, Jumamosi iliyopita katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.

Club Africain ya Tunisia baada ya kutambiwa vikali na TP mazembe, iliweza kutoa wito kwa wachezaji wake wote kuweza kupimwa vipimo ili kutazama labda kuna sumu waliweza kupewa huko Lubumbashi.
 Club Africain inashutumu TP Mazembe ya kuwapa sumu wachezaji wake katika chakula chao. Mashtaka hayo yalitangazwa na kiongozi wa timu hiyo huku majibu ya vipimo ikiwa tofauti na madai hayo.
Mkurungezi wa michezo ya TP Mazembe aliweza kuandika kwenye akaunti yake ya Twitter, akisema kuwa sumu haiwezekani. "Club Africain walichagua pekee yao hoteli na walikuja na chakula na maji yao. Alimalizia Frédéric Kitengie 

katika tovuti ya TP Mazembe, iliweza kuandika : Kujua kukuali kushindwa pia ni ukubwa wa klabu.

Inaonekana Club Africain inachanganyikiwa na matokeo wakati kuna sheria za ushindani, kwa hiyo CAF inaweza  kuadhibu klabu ya Tunisia endapo hawatakubali kushindwa.

Mchezo wa marudio ni mnamo Februari 12  huko Tunis.

Hakuna maoni