News | Yafichuka B Bright kaiba mashairi ya Driss kaitumia kwenye wimbo wake So Good
Inasemekana msanii B Bright kamwibia Driss baadhi ya mashairi pamoja na idea mzima ya nyimbo yake So Good.
Driss alishangazwa kusikia B Bright kaachia wimbo mpya wakati baadhi ya mashairi zinazo beba track So Good ni za kwake, track ya Driss inasemekana haijatoka, anatarajia kuiachia hivi karibuni.
Driss alisema kwamba walifanya kazi pamoja na B Bright inaitwa ''Shalom'',
''Niliwahi kufanya naye wimbo unaitwa Shalom, nilimuona kama ni rafiki mzuri baadae nikarudi studio kutengeneza track yangu itakayobeba jina la Umutima. B Bright ni kama rafiki alinisindikiza studio inaitwa Kigazi Arts Record kwa King Plata, nilitunga mashairi pekee yangu na nikaanza kuimba hapo hapo kumbe kijana ni mwizi kaiba mashairi yangu na kujifanya mjanja kutoa mbele yangu. Kiukweli vesi ya pili ya wimbo wake So Good ni mashairi yangu na pindi wimbo wangu utatoka hivi karibuni utaamini.'', Alisema Driss kwa unyonge.
''Kama tayari ulisikiliza kwa makini wimbo wake So Good kuna vesi ya pili kaimba hivi, Tatu y'izina ryawe iri kumutima
Let me be your one two maze nkubere umuco mumwijima
Fatu ubwiza bwawe butuma je nishima
Ntitugire pas du tout urukundo rwacu rumere nk'isinema, hayo ni mashairi ambayo nilitunga na inapatikana kwenye wimbo wangu Umutima'', alimalizia Driss
Post a Comment