MISHE-BOY

Sport | Sababu ya Shaka Bienvenu kujiunga na Etoile du Sahel kuliko Club Africain

Mshambuliaji wa timu ya taifa Burundi, Shaka Bienvenue amesaini mkataba wa miaka mitano na Etoile Sportive du Sahel baada ya kufanya majaribio katika klabu Club Africain bila mafanikio.

Baada ya siku chache za kupima  kwenye Club Africain, mshambuliaji wa Burundi Shaka Bienvenue hatimaye alijiunga na klabu nyingine mpya ya Ligue 1 inchini Tunisia.
Akiwa bado mdogo mwenye umri wa miaka 19, alikuwa mchezaji wa klabu Aigle Noir na alikuwa alifunga mabao 29 msimu uliopita.

Kwa mjibu wa baadhi ya majadiliano, mshambuliaji mrundi alicheza mchezo wa kirafiki na Club Africain dhidi ya klabu Garatasaray ya Uturuki, kocha wa Club Africain, José Riga hakupendezwa na kiwango cha Shaka na kuamua kukataa kumsajili moja kwa moja.

Baada ya siku mbili, Shaka alikubali hofa ya Etoile Sportive du Sahel kwa kusaini mkataba wa miaka mitano.

Hakuna maoni