MISHE-BOY

News | Sat B akubaliwa collabo na Sauti Solo

Kundi la Muziki maarufu Afrika Mashariki kutoka Kenya, Sauti Solo iliwasili nchini Burundi Agosti 02, kwa mara ya pili kwa kukamilisha tamasha yao jijini Bujumbura.

Katika maojiano na waandishi wa habari, Sauti Solo ilisema kwamba nchi ya  Burundi wanaichukulia kama nchi ya pili kama wako nyumbani ndio maana wanaendelea kutembelea Burundi na tayari wamekuwa warundi.
Sauti Solo ni kundi inayofanya vizuri Afrika mashariki na duniani, wamemtaja Sat B kama ni msanii anayefuata kwenye orodha ya wasanii watakao fanya nao  kazi na walisisitiza kwamba hawataondoka hawajakamilisha collabo hiyo.

Staa wa muziki wa Buja fleva, Sat B ameweka wazi kuwa ana hamu ya kufanya kazi na Sauti Solo, bila shaka waliondoka kwenye Conference mchakato ukiendelea kimya kimya.

Sat B ambaye jina lake linazidi kupata umaarufu nchini na nje ya nchi kutokana na nyimbo zake kadhaa kama FEEL LOVE, NO LOVE na zingine nyingi kibao, aliweka wazi mbele ya waandishi wa habari na kutaja jina la wimbo litakalo fuata baada ya Feel Love na No Love labda ikawa ndio jina la wimbo ya collabo yake na Sauti Solo ni LOVE CONTROLER.

Hakuna maoni