MISHE-BOY

Sport | Papy Faty anasema haogopi kitu licha ya maswala yake ya awali ya afya

Mchezaji wa timu ya taifa Burundi amejiunga na New Real Kings ya Afrika Kusini, Papy Faty alisema haogopi kitu na atahakikisha amerudi kwenye kiwango chake licha ya maswala yake ya awali ya afya.

Papy Faty  akiwa na kandarasi hivi karibuni  ya miaka miwili na Real Kings baada ya kufanya vizuri miaka miwili na Wits Bidvest.
Mwenye umri wa miaka 27, alionyesha kuwa hana madhara yoyote baada ya kuonesha kiwango kizuri  katika Kombe la KZN Premier ya mwishoni mwa wiki hii iliyopita kwa kufunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Amazulu na Uthongathi.

Alipoulizwa kuhusu muonekano wake na uchezaji wake wakati alikuwa nje ya uwanja miezi kadhaa, Papy Faty alisema :
"Unajua wakati mwingine unaweza kuchukua maamzi mazito ila kama unaweka niya mwenyewe kufanya hivyo, unahitaji kwenda njia yote. Kwa kuwa mimi ni mtu wa Mungu siwezi kuogopa chochote. hata pakiwa baadhi kunitisha naona kama hawata faulu katika hili tayari naweza kucheza dakika 90 na nimeifanya dhidi ya Amazulu katika nusu fainali.


"Nitaendelea mpaka  hadi mwisho wa msimu. kwasasa niko sawa ata kucheza michezo yote ila inategemeana na uamuzi wa kocha.
"Kwanza, kocha ana uaminifu kwangu na yeye ndiye sababu ya mimi kuwa hapa, ameniita ameona  kama nafaa na akaniunga mkono, naye ameona kuwa hakuna ishara yoyote ya kutisha kwajili ya afya yangu.

Kwasasa nacheza kila mchezo wa kirafiki nacheza dakika 90. Baadhi ya michezo ninayoenda kwa dakika 120. Ninajisikia kama niko tayari na nitakuwa bora zaidi kwa msimu wote kwa timu hii. "

Hakuna maoni