MISHE-BOY

Sport | Sababu kubwa ya Zidane kuondoka Real Madrid

Kwasasa habari ya Kocha mkuu wa Real Madrid ya Hispania kujiuzulu inazidi kushangaza watu wengi duniani pote baada tu ya kutwaa kombe la Ligi ya Mabingwa mara tatu mfululizo.

Sauti ya radi imeiangukia Real Madrid kwa kuweka mshangao kwa kila mtu pale Zinedine Zidane aliwahita waandishi wa habari na kutangaza kuondoka Real Madrid, uamuzi husiotarajiwa kabisa, ambao umesababisha wachezaji wengi wa soka kuguswa kuanzia wachezaji wa Madrid.

Zidane alijiakikishia mwenyewe kwa kueleza kwamba REAL MADRID ILIHITAJI MABADILIKO, gazeti la AS imegundua kuwa hii ni moja ya sababu iliyosababisha Zidane Kujiuzulu.

Kwa kweli mfaransa Zizou hakupendezwa na mtazamo wa kiongozi wa Madrid, Florentino Perez katika siku za hivi karibuni.
Kiongozi wa Real Madrid amechukua uamuzi wa kukataa kulipa faini kubwa iliyopatikana na Cristiano Ronaldo na akasema yuko tayari kumuuza mreno endapo ataendelea kumsaliti.

Aidha, Floretino Perez pia alijaribu kumuomba Zidane awe na mazowea ya kumtumia sana Gareth Bale ili aje kuwa mchezaji wake muhimu msimu ujao kuliko Cristiano Ronaldo.

Bila shaka amri hizi hazikumpendeza sana Zidane na kuamua kujiuzulu kwa kile ambacho mfaransa alidai kwamba kwasasa timu ya Real Madrid inahitaji ''mabadiliko''.

Hakuna maoni