News | Natacha ni bora kuliko wote Burundi asema Bien Freema
Baada ya mashabiki kuona huenda Big Fizzo ndiye msanii bora zaidi Burundi, kwasasa kuna utofauti wa vigezo vinavyomfanya mwana mama Natacha a.k.a La Namba Natacha Nomaa kuwa bora kwa wasanii wa Buja Fleva.
Ni mjadala mpana katika mitandao ya kijamii, mitaani na hata miongoni mwa wasanii wenyewe ambao kwa kificho au waziwazi wameanza kuona msanii anaezidi kufanya vizuri zaidi tofauti na wale wasanii waliyoanza kuingia na kupata jina katika muziki wa Buja fleva.
Katika miaka za nyuma akiwa na singo yake Unaniongopea akishirikiana na kundi nzima ya Bongo Fleva, Ya Moto Band ndiyo iliyomfungulia milango kimataifa na baadae akaachia tena singo yake Shikilia iliyomfanya kudumu mda mrefu huku alizidi kufunika alipo shirikiana na mrembo wa Uganda Sheebah katika wimbo wake uitwao Wangu.
Natacha kutoka Burundi mafanikio yanayomfanya kuwa mbali na ki ubora kwa kumlinganisha na wasanii wengine.
Kwa fikra yake mwenyewe, Natacha aliandaa tamasha Burundi Bwacu Tour na kupewa nafasi ya kutumbuiza kwenye matukio makubwa nchi nzima, nani Mwingine?
Kwasasa anapatika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa kukamilisha wimbo wake akiwa pamoja na nyota wa nchi hiyo, Fally Ipupa. Bila shaka hiyo ni dalili ya kukubalika na wasanii wa kimataifa.
Kufanya wimbo na Fally Ipupa itamsaidia Natacha kujulikana zaidi na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wakubwa Afrika.
Licha ya wasanii wengine wa Buja fleva kuzunguuka Ulaya, wanashindwa kutumia mda huwo nkwa kufanya kazi na wasanii wa nje wenye uwezo mkubwa ili waweze kuwasaidia kuingia katika soko la Ulaya.
Msanii wa muziki nchini Bien Freema alifunguka kwa kukubali kama Natacha kwasasa anatarajia kuwa msanii bora zaidi nchini,
sikiliza Hapa :
Post a Comment