MISHE-BOY

Sport | Nchi 11 ambazo zimeisaliti Morocco

Nchi ya Morocco imekua miongoni mwa wagombea wa kuwania kuandaa wa Kombe la Dunia ya 2026, iliangushwa na Muungano wa Umoja wa Mataifa ( USA-Mexique-Canada) ambao ilipata 67℅ ya kura katika kura ya FiFA.

Baada ya kupokea kura 65 tu kutoka kwa shirikisho za soka 203 walioalikwa kupiga kura, Morocco umeshindwa kushinda kwa mara ya tano katika historia yake ya kuwania kuandaa mashindano hayo.

FIFA imeweka wazi maelezo ya kura ya nchi na nchi na kuweka wazi faili ya Morocco kutokufanya vizuri. Kwa kweli nchi 42 tu kwa nchi 53 za CAF waliipa sauti zao kwa nchi ya Morocco.

Nchi 11 ambazo zilipendelea kuunga mkono Amerika ya Kaskazini badala ya kuona Kombe la Dunia kwa mara ya 2 ifanyike Afrika ni Benin, Botswana, Cape Verte, Guinea, Lesotho, Liberia, Namibia, Msumbiji, Sierra Leone, Afrika Kusini na Zimbabwe.

 Ikumbukwe kwamba Guinea imethibitisha kuwa imetoa kura yake kwa Morocco.

Hakuna maoni