MISHE-BOY

Newz | Natacha asaini mkataba mnono na kampuni ya Tanzania



Staa wa Buja fleva nchini Burundi, Natacha a.k.a La Namba Natacha Nomaa amesaini mkataba Juni 11, 2018 na Kampuni Kwetu Studio ya nchini Tanzania.

Baada ya ziara yake ya siku chache DR Congo kwa kukamilisha kolabo yake na Fally Ipupa, ametua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba wa miaka miwili na Kwetu Studio inayojihusisha na utengenezaji wa video.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Mwanamama Natacha amesema anashukuru kupata mkataba na kampuni hiyo.

Aidha, Kampuni hii kubwa ya muziki Afrika Mashariki, itasimamia video zake  na audio  kwa kuzifikisha kwenye masoko makubwa ya muziki duniani pote.

Kwa sasa kazi za Natacha zitasimamiwa Kwetu Studio duniani kote  ambao watasimamia kazi zake  kwa kiwango cha kimataifa zaidi na bila shaka hiyo ni moja ya vitu watafanya.

Hakuna maoni