MISHE-BOY

News | Vitu Lady Jay Dee hapendi kuzungumzia kwenye Media

Mwanamuziki wa kike wa Bongo Fleva kutoka Tanzania, Lady Jay Dee pamoja na kuzungumziwa mara kidogo ishu yake ya ndoa kwenye social media, alifunguka mbele ya waandishi wa habari nchini Burundi katika maojiano ya kuandaa show yake siku ya Laidi.

Jay Dee amesema kwamba hivi karibuni amekua haongei sana na media na hapendi kuulizwa kuhusu maisha yake binafsi.

Hata ukiangalia akaunti zake za social media  kama page, instagram na zingine haposti maisha yake binafsi tofauti na wasanii wengine nchini hapo.

Moja ya sababu wasanii wachache hawpendi kuposti mambo yao binafsi, wanaamini kuwa unaposti ndugu, mzazi, mchumba au mme ni unawaweka kwenye situation ya watu kuanza kuwaongelea na watu wengi wanaweza kuongea kitu chochote kile kwa hiyo kutokuongelea vitu binafsi ni kupenda kuwalinda watu ambao wako karibu yao.

Moja ya maswali ambayo ukimuuliza Jay Dee hatokujibu wala kuongelea chochote ni ishu ya uhusiano wake wa kimapenzi na endapo atakujibu bila shaka jibu yake ni MAMBO BINAFSI ITAKABI KUWA BINAFSI NA SIO YA KUONGELEA KWENYE MEDIA.

Hakuna maoni