MISHE-BOY

Sport | Kara Mbodji anaweza kuikosa Kombe la Dunia 2018

Habari hii inaanguka kama pigo kwa timu ya taifa ya Senegale, alipoitwa kuulizwa kwa kuumia kwa Kara Mbodji na upasuaji wake, Kocha wa Anderlecht, Hein Vanhaezebrouk alisema '' Kara anapaswa kuwa nje ya uwanja mpaka mwisho wa musimu na kuna uwezekano wa kuikosa Kombe La Dunia 2018''.

Baada ya kuumia kwenye goti, kara Mbodji alifanyiwa upasuaji Desemba iliyopita na alikaa nje ya uwanja miezi miwili tu. Lakini mchezaji wa kimataifa ya Senegal anazidi kupata tatizo kila kukicha kwenye goti yake, kwa mjibu wa taarifa ya Kocha wa Anderlecht alisema kuwa afya ya mchezaji si nzuri '' inakuwa wiki 8 akiendelea kupata matibabu nchini Hispania na bado hakuna mabadiliko mema, hajakuwa tayari kucheza mechi yoyote'', alisema Vanhaezebrouck. 

''Kara anakuwa na hofu, alifikir kama anaweza akapona na kurudi kucheza  mapema, lakini anaweza kuikosa Kombe la Dunia kwasababu ya hiyo'', alisema kocha wa Anderlecht.

Hakuna maoni