MISHE-BOY

Sport | Manchester City kupigwa faini ya £ 50,000 na FA?

Shirikisho la Soka la Uingereza lilipiga faini  Manchester City kwa Tabia mbaya baada ya wachezaji wa timu hiyo kupigana kwenye chumba ya mapumziko katika mechi ya Cup dhidi ya Wigan (1-0).

Timu inayoongozwa na Pep Guardiola, Manchester City ilipokea barua  nzito kutoka kwa Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) adhabu ya pounds 50.0000 kwa ugomvi uliyofanyika muda mfupi kabla ya mechi ya Cup dhidi ya Wigan (1-0,  kwa ushindi wa Wigan) kufuatia mchezaji Fabian Delph.

Baraza linaloongoza Soka la Uingereza lilisema : '' Manchester City inapigwa faini ya pounds 50.000 baada ya kushindwa kudhibiti wachezaji wake.'' Baada ya uchunguzi baraza hilo limetoa maamuzi yake Machi 02, 2018.

Tukio hilo limefanyika katika mechi ya kufuzu  Kombe la FA Cup mwezi uliopita dhidi ya Wigan Athletic. Delph amepata kadi nyekundu baada ya kumfanyia kosa mchezaji wa Latics Max Power.
Pep Guadiola na Paul Cook, kocha wa Wigan pia walitupiana maneno makali katika eneo la kiufundi na kisha kwenye makanda ya uwanja huo.
Mshambuliaji wa Argentina pia alianza kupigana na wachezaji wa Wigan mwishoni mwa mechi hiyo.






Hakuna maoni