Newz | Gaga amdiss Big Fizzo kwa video yake na kuipaisha video yake
Msanii wa muziki wa Burundi Fsleva, Gaga Blue ambaye anatikisa hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii na video ya wimbo wake mpya ''Mama la Mama'' aliyowashirikisha wasanii wa Bongo fleva, Mr T Touch na Barakah the Prince, inadaiwa ameonesha diss ya wazi kwa video ''Konzi'' ya Big Fizzo na kuipaisha video yake.
Ameonekana mjini dar e salaam leo asubuhi akizunguukwa na waandishi wa habari wakimuoji maswali kuhusikana na uwepo wa producer Mr T Touch kuimba kwa mara yake ya kwanza kwenye wimbo wake tofauti na jinsi wanavyo mfahamu.
Gaga Blue alisema kuwa yeye ndie alimsababisha producer huyu kuimba na ameonekana kama anaweza pande zote na kuongeza kuwa Mr T Touch anakipaji cha hali juu.
Aidha video yake imeachiwa siku moja na video ya Big Fizzo, msanii huyu alisikika akitamka na kuweka wazi diss kwa video ya Fizzo na kusema ,
'' napenda sana kufanya kazi zangu hapa kwasababu na jifunza mengi sana na kwasasa insu ya 1k viewz kwa siku chache sio tena tatizo kwenye video zangu, nasikia home wanashindana kwa viewz kama watoto wadogo ila tazama video yangu ya mama la mama inaiacha kwa mbali zaidi video ya Konzi ambayo tumeachia siku moja baada ya mwingine, itakuwia wepesi kubaini namna ''Mama la mama'' inavyofunika ''Konzi'' kibiashara. Twende mdogomdogo''.
Alipo ulizwa kwanini analinganisha video yake na ''Konzi'' na wametaka kufahamu konzi ni video ya msanii gani kutoka Burundi, Gaga Blue alijibu na kusema,
''huyo ni mwanamuziki ambaye madhumuni yake ni kuimba nyimbo nzuri ili awe anasikilizwa na marafiki zake au na nduguze halafu wanaburudika, mimi sivyo''. alimalizia Gaga Blue.
Post a Comment