MISHE-BOY

Newz | Huyu ndie producer wa Bantu Boy Record ya Big Fizzo


Staa wa muziki wa Burundi Fleva, Big Fizzo siku za nyuma alitambulisha mradi wake mpya kwa picha kadhaa zikionesha anatarajia kutuletea studio yake mpya ambayo inabeba jina la Bantu Boy Record.

Wengi wameanza kujiuliza maswali mengi na kutaka kumtambua producer atakae jiunga na Studio hiyo na kufanya kazi nzuri.
Orodha ya ma producers wanao fanya vizuri nchini imeanza kutajwa ila boss wa studio hiyo ambae ni Big Fizzo leo hii alipost picha ya Producer mahiri nchini  kwenye ukurasa wake wa facebook  na kuandika ''Breaking newz d j wa Bantu bwoy record ni the baddest producer who produced #konzi Yves kolly .welcome in the family man''.
Bila shaka producer atakaeanza kazi kwenye studio hiyo ni yule yule producer anaefanya vizuri nchini pia akiwa mwanamuziki mzuri  akifahamika kwajina la Kolly The Magic.

Tuwakumbushe kuwa Kolly ndie producer aliyetengeneza wimbo ''Konzi'' ya Big fizzo ambae ndie boss wake kwa sasa. 

Hakuna maoni