MISHE-BOY

New | Tayari Director wa Hello ya Best Life afahamika

Kundi la Muziki ya Burundi Fleva, Best Life ambao inazidi kufanya vizuri kwenye ulimwengu wa muziki wa kizazi kipya, ilitangaza tarehe rasmi ya uzinduzi wa video ya wimbo wao mpya ”Hello”  hivi karibuni.

Baada ya kuachia lyrics ya wimbo ”Hello” kilicholeta mashaka na wapenzi wa burudani hapa nchini kwa kufikiria labda ndio mwisho hawatapata video ya wimbo huwo mzuri. Kundi la Best Life Music hivi karibuni hitarajia kuachia video ya wimbo yao ”Hello” ambayo inatarajiwa kuwa mitaani kuanzia tarehe  10  mwezi Februari  kuwa kuondoa shaka kwa wapenzi wa muziki.
NGM257 ilipata fursa ya kuongea na msimamizi wa kundi hilo, Kent P ambapo alidai kuwa Video imekwishakamilika kinachosubiriwa ni mda wa kuitupa marikiti kwani inaaminiki kuwa mashabiki wana kiu kubwa sana kuona kazi nzuri kutoka kwa watoto wa Burundi.

Wengi wamezowea kuona video ya kundi hili ikisimamiwa na director Kent P, kwa ujio huu mpya wa video hiyi, director ametambulika kwa mjibu wa Kent P akisema : 
 ”Imeshazoeleka kuwa mapanga ndio staili bora kabisa nchini hasa unapolitaja kundi la Best Life Music lakini safari hii  wanakuja na staili mpya  “ili kuonesha kuwa sisi hatupimiki tumeamua kuja na staili mpya kabisa za muonekana na kufanya video za kimataifa pamoja na director mkubwa ambae bila shaka wengi wanamfahamu ni Sasha Vybz kutoka Uganda, mbali na hiyi video nyingine kibao  zitakuwa ni surprise kwa mashabiki'”. Alisema msemaji wa kundi best Life Music, Kent P.

Tuwakumbushe kuwa mpaka sasa Kundi hili wanatamba na ngoma zao ’ zinayobeba jina la ” Hello, Your Vodo pamoja na Overdose”.

Hakuna maoni