MISHE-BOY

Mchezaji mrundi nzokira jeff na kocha Amars waibuka washindi wa kombe la nchini Djiboutie msimu huu


Ligi Kuu ya Djiboutie imemalizaka hapo tarehe 4/05/2015, baada yakuongoza kwenye msimamo wa ligii Kuu kwa muda mrefu wakiwa wakikimbizana kwa kugombania  ubingwa msimu huu na klabu pinzani As Port. Klabu ASS Telecom Djibouti inayo ongozwa na kocha mrundi Amars pia ni ya mchezaji mrundi Nzokira Jeff aliye kuwa golikipa wa klabu ya Vital'o Fc ya mjini Bujumbura, imekuwa  wa bingwa msimu huu kwa mara tatu mfululizo.
 Tarehe 04/05/2015 klabu ya kocha mrundi Amars imekuwa inachuana na Jajago Fc na kuicharaza vibaya sana klabu iyo  Jajago Fc kwa bao 9 bila (9-0), mechi wameikania sana kwasababu ilikua nimechi ya kupata ushindi bila ivo matumaini ya kuchukuwa kombe msimu huu imekuwa ndogo sana.
Kwa ushindi wao wa bao 9 bila na kumaliza na pointi 45, goli 62 wamenyakuwa kombe msimuu huu 2015, golikipa mrundi Nzokira jeff mwaka huu amefungwa goli 15 tu na kumuweka na fasi pazuri sana kama golikipa bora kwa miaka mitatu.
 Mchezaji bora ni mchezaji wa klabu ya kocha Amars ambae anajulikana kwa jina la Mouhamed Jama Oubayo. Kuna mchezaji umoja amewayi kuichezea klabu ya Lydia Lydic Academic anaye julikana kwajina la Andosango freddy ameibuka na kumaliza msimu wake mwaka huu na goli 9.
Upande wa kocha Amars mwaka huu ndio mwaka wake wa kwanza kuikochi klabu iyo ya ASS Telecom Djibouti na amechukuwa kombe mbili msimu huu, moja ni Super Cup na Ligi Kuu ya Djiboutie 2015.
habari nzuri tena ya kupendeza ni kwa golikipa mrundi Nzokira Jeff ambae kwasasa ni miaka nne (4) amekwisha ipatia klabu yake kombe tanu (5),  Kombe mbili ya Super Cup na Kombe tatu (3) ya Ligii kuu Ya Djiboutie.
Kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mchezaji Nzokira jeff ameonesha ishara kubwa sana na kusema;
'' nawashukuru sana mashabiki wangu wa Djiboutie na Burundi pia, kwasababu sapoti yenu ndio inazidi kunipa bidii ya kuzidi kufanya mambo mazuri kwenye klabu hii, na ninazidi kuongeza nguvu ili  mzidi kunikubali kama gisi klabu yangu inavyo nikubali na pia nazidi kupeperusha bendera ya Buurundi nikiwa nje ya nchi yangu baadae na kuja nyumbani tuchangie chai chapati braaah.'' alisema Nzokira Jeff.
 

Hakuna maoni