MISHE-BOY

CAN 2017 Senegal vs Burundi, timu ya taifa ya Burundi inapewa bahati kwa kufanya vizuri



Timu ya taifa intamba murugamba ambao  inaendelea  vizuri sana kwa kujiandaa mechi dhidi ya Senegal mjini Dakar kwa kugombania kufuzu kwa Can 2017 nchini Gabon. Timu ya taifa Intamba Murugamba imewasili vizuri sana mjini dakar kwamjibu wa mtandao Afrifame. Orodha ya wachezaji ambao imetangazwa awali na  kubaki na wachezaji 23 ambao watawakilisha Burundi kwenye michuano ya kufuzu kombe la Afrika Can 17 nchini Gabon. orodha ambao imewasili Senegal kwa mechi ya kwanzakwa kufuzu Can2017 nchini Gabon uku timu ya taifa Intamba Murugamba ikiwakilisha Burundi bila wachezaji wake vigogo kama Ntibanzonkiza Saido , Papy Faty, Nzokira Jeff, Didier Kavubangu, Amissi Cedrick nawengineo wengi ila stamina ya wachezaji ambao wamejielekeza Senegal ni nzuri sana.

Burundi:

1,BIHA Omar / Vital'o Fc
2. RUGUMANDIYE Yvan / Muzinga
3. KIZA Fataki / LL s4a
4. NKURIKIYE Leopold Kaya / Vital'o Fc
5. HARERIMANA Rashid Leon / LL s4a
6. Idi DJUMAPILI / Vital'o Fc
7. NSHIMIRIMANA David / Vital'o Fc
8. RUGONUMUGABO Stepfane / LL s4a
9. BARENGE Pistis / Vital'o Fc
10. MOUSSA Mossi Hadj / Vital'o fc
11. NAHIMANA Shassir / Vital'o Fc
12. Hussein SHABANI TSABALALA /Vital'o fc
13. DUHAYINDAVYI Gael / LL s4a
14. BIZIMANA Hassan / Inter star
15. NDARUSANZE Claude / Gunners Fc - Bostwana
16. TAMBWE Amissi / Yanga Africans
17. Fiston ABDOUL Razzak / Sofapaka kwasasa amesaini mkataba na  Mamelodi sundowns ya Sauza Afrika
18. Laudit MAVUGO / Vital'o fc.
Timu ya taifa ya Senegal imeweka wazi orodha ya wachezaji wake ambao wataweza kuchuana na Burundi mjini Dakar tarehe 13 Juni saa 20:00 katika uwanja Leopold Senghor. Timu ya taifa ya Senegal itapambana na Burundi wakati kuna baadhi ya wachezaji nyota awatakuweka kama Papy Djillobodji, Dame Ndoye, na Moussa Sow ambaye ni mfungaji mzuri na kwasasa amekwisha ifungia klabu yake mabao 17, Kukosekana kwa Papiss Cissé imeleta mushangao mkubwa sana kwasababu mchezaji amerudi kwenye kiwango chake baada ya kuumia siku chache.  Kwa ukosaji wa hao wachezaji  wa Senegal inaiweka Burundi kuwa na imani ya kufanya vizuri kwenye mechi yake ya kwanza kwa  kufuzu kwa Can 2017 nchini Gabon . Mchezaji mpya kabisa kwenye orodha ya Senegal ni  Amara Baby mshambuliaji wa JA Auxerre ambaye amecheza mechi ya mwisho ya kombe la ufaransa ( Coupe de France) dhidi  ya Paris Saint-Germain,.Hatimaye, Victor Bindia Alioune Ndiaye na Pape, na Henri Saivet wamerejeshwa kwenye hii orodha ambao itakao pokea timu ya taifa Intamba Murugamba. Mechi Senegal / Burundi kwa siku ya kwanza ya kufuzu kwa CAN 2017 nchini Gabon, itafanyika mjini Dakar tarehe 13 Juni saa 20:00 katika uwanja Leopold Senghor.

Hakuna maoni