MISHE-BOY

Papy Faty anazidi kumushangaza kocha wake kwa kiwango chake kuzidi kuongezeka kwa kila mechi



Mchezaji mrundi Papy Faty tangu arudi kwenye klabu yake ya FC Bidvest Wits baada ya kukaa miezi kazaa uku akisumbuliwa na maumivu iliyo mpata kwenye mechi ya ligi Kuu ya Sauza Afrika ijulikanao kama PSL dhidi ya klabu Orlando Pirate tarehe 19 mwezi wa 5 mwaka wa 2014.  Ivi amepata nafuu na amekwisha udhuria mechi 3 uku akionesha kiwango kikubwa sana mpaka mashabiki na kocha wake kumpongeza sana na kwa sasa ni mgawaji bora kwenye timu yake.

Papy Faty ni mchezaji ambae anazidi kuleta mchango mkubwa sana kwenye timu ya taifa uku akiwashawishi wachezaji wenziye ambao awana niha n yakuja kujiunga na kuichezea timu yao ya taifa Intamba Murugamba ili waje na wasaidie nchi yao ifaulu kupata tiketi ya kucheza kombe la Afrika.
Ivi leo tarehe 03/03/2015 klabu yake imepata nafasi kubwa sana ya kufaulu kupata pointi 3 dhidi ya klabu pinzani Mamelodi Sundows ambayo  imekua inachukua na fasi ya 2 uku klabu ya mrundi Papy Faty, Wits ikichukuwa na fasi ya 3.  Saa moja na nusu tarehe (19h30) tarehe 03/03/2015 ndio Timu ya mrundi Papy Faty imeteremka uwanjani  uku Papy Faty akiwa kwenye ile kumi na moja uku akiitendea haki klabu yake na kudhibiti mechi mwanzo mpaka mwisho bila kasoro. Mechi imekwisha kwa ushindi wa klabu ya mchezaji mrundi Papy Faty kwa bao moja zero (1-0) kwa faida ya Wits, na kujiweka na fasi ya pili kwenye msimamo wa ligi PSL. Ijumaa tarehe 06/03/2015 klabu ya Papy faty, Wits  inapambano nyingine tena kubwa sana dhidi ya blomfontein celtic  kwenye uwanja wa bidvest ijulikanao kama  millpark stadium saa moja  19h30 gmechi  ya league PSL.
Baada ya mechi Papy Faty ameonesha furaha uku akiwa na hamu kubwa sana ya kurejea kwenye timu ya taifa na kucheza mechi mwaka huu kwa sababu hapa akisema:

''niko fiti na ninaendelea poa kila mtu anaona gisi ninavyo cheza mpaka kocha kufikia kunisifu ni jambo nzuri sana ila napenda ufiti huu udhiririke kwenye timu yangu ya taifa Burundi''.

Hakuna maoni