MISHE-BOY

Nzokira Jeff "Double Man" ndio jina wanayo muita Djiboutie

mchezaji Mrundi, Nzokira Jeff ambae anaye ichezea klabu ya A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM ya nchini Djiboutie. ivi karibuni klabu yake imekabidhiwa ao imetawaziwa ubingwa wa musimu huu kwa mara mbili mufululizo. tukumbuk kuwa aliwahi kuichezea nchi ya Burundi kwenye timu ya taifa ya Intamba Murugamba na kwenye klabu ya Burundi Vital'o, amepata sifa nyingi barani afrika na nchini Burundi kwa kupata kombe nyingi na klabu yake ya Vital'o Fc. ndipo amesajiliwa na klabu ya Djiboutie, kwa sasa mambo yake na stamina inazidi kuongezeka zaidi sana.
Tuwakumbushe kuwa klabu ya A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM imekwisha chukuwa kombe mara 3 (2009-2010,2012-2013 na 2013-2014 ) ya ligi kuu ya Djiboutie, ndipo walisajili wachezaji wenye mahiri sana na wakaja kumchukuwa Jeff kwa ule msemo wa Raisi wa klabu iyo ''Pour être champions il faut commencer par recruter un TRES bon gardien".anamaanisha kuwa kwakuweza kuwa bingwa inabidi kuanza kusajili golikipa mzuri (Nzokira Jeff) ndio lengo lao wamemsajili Nzokira Jeff na ameweka historia ambao akuna golikipa wowote amewahi kuweka nchini Djiboutie ya kuwa golikipa bora miaka 2 zakufatana na kufungwa goli chache sana kama 2 kwenye Michezo yote ya Ligi kuu.
kwa upande wa Nzokira Jeff amechukuwa kombe 3, yaani kombe 2 ya ligii kuu ya Djiboutie 2012-2013 na 2013-2014 yaani huu Mwaka. na moja ya Super cup mwaka wa 2011. kwa kuchukuwa kombe 2 mfululizo, wamempa jina la Double Man.
hapo jana tarehe 11/04/2014 ndipo wamekabidhiwa kombe na uku wakisherekeya kwa furaha sana. mchezaji Nzokira Jeff akibebelewa bendera ya nchi yake na kuweza kuonesha kuwa Burundi wanaweza ki soka na amewakilisha nchi yake vizuri sana ugenini.
sipekee yake kwenye hiyo klabu kuna mchezaji pia amesajiliwa akitokea Burundi kwenye klabu ya LLB Academic, ni Andosango Freddy, amejiunga na  A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM msimu huu wa 2013-2014, kwa bahati nzuri mwaka wake wa kwanza na kusaidia klabu ya A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM kupata kombe kwa mara yake ya kwanza akichezea.
Andosango Freddy
ebu cheki picha za sherehe ya kukabidhiwa kombe ya klabu A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM na sherehe kamili ya klabu itafanyika hapo siku ya ijuma nne tarehe 15/04/2014.
Freddy  na Jeff (Burundian)
Jeff akiwa na Viongozi wa A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM
Bendera ya Burundi inazidi kupepeya
Jeff akishangilia kwa furaha uku Bendera aitoki shingoni pake
picha ya pamoja na kuzidi kutangaza Nchi yake
Jeff akiwa na mwenye kiti wa A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM
Ongera sana kwa Nzokira Jeff na Andosango Freddy, kwa kuitangaza nchi yetu ya Burundi.

Hakuna maoni