Sport | Gabon yamtambulisha rasmi Daniel Cousin na Pierre Aubame kuchukua nafasi ya Camacho
Baada ya kumtimuwa kocha wao kutoka Hispania, José Antonio Camacho wiki iliyopita, hatimaye Gabon imewatambulisha Pierre Aubame na Daniel Cousin kama makocha wapya wa timu ya taifa Gabon.
Mambo sasa yanazidi kuwa sawa katika mji wa Libreville, siku chache baada ya kumtimua Antonio Camacho, Gabon ilitangaza Jumatano kocha wake mpya au tuseme Duo mpya ambayo inajumuisha na Pierre Aubame, baba wa Pierre-Emerick Aubameyang na Daniel Cousin.
Hawa wawili wachezaji wa zamani wa timu ya taifa Gabon, wana sifa kubwa na uzoefu wa ushindani wa kiwango cha juu kwa uzoefu wao huwo na kujua hali halisi ya timu hiyo.
Kwa niya ya kufuzu Kombe la Afrika CAN2019 huko Cameron, Gabon inalazimika kufanya vizuri katika michezo miwili dhidi ya Sudan ya Kusini.
Post a Comment