MISHE-BOY

Sport | Bao pekee ya Berahino na sare ya Burundi, yamfukuzisha kocha wa Gabon

Kama ilivyotarajiwa José Antonio Camacho sio tena kocha mkuu wa Gabon,  baada ya kushinda kuiongoza timu hiyo kuwa na fursa ya kushiriki Kombe la Afrika mwaka ujao wa 2019 nchini Cameron. Mhispania huyo alifukuzwa kabla ya miezi miwili ya mwisho wa mkataba wake.

Kati ya José Antonio Camacho na Gabon mambo kwisha kama ilivyo thibitisha vyombo vya habari nchini hapo.

Kwa mjibu wa Waziri wa michezo wa Gabon Alain Claude Bilie-By-Nze alisema Jumatano hii kwamba Camacho sasa amepoteza nafasi yake ya kufundisha baada ya kutoka sare na Burundi katika wiki ya pili ya kuwania kufuzu Kombe la Kimataifa CAN 2019 na Kocha mwingine atachukua nafasi yake kwenye benchi ya Gabon mwezi ujao kwa mapambano mawili dhidi ya Sudan Kusini.

''Niliita Fegafoot (Shirikisho la Soka la Gabon) asubuhi hii kuonyesha kwamba hatukubali matokeo mabovu ya timu ya taifa'' , alisema  Kiongozi huyo.

''Nimechukua uamzi wa muda mfupi ili asijali timu kwa michezo ijayo kwa sababu Mheshimiwa Camacho ana mkataba hadi Novemba, sasa nafikiri tunaona kama tuna shida katika timu, tunapashwa kuzibadili na wakati kocha ni sehemu kubwa ya shida hiyi, lazma tutatuwe.''

Licha ya kusaini mkataba mnamo Novemba mwaka wa 2016, mwenye umri wa miaka 63,  Camacho alishinda michezo miwili, sare 8 na kushindwa michezo 7 katika michezo 17. Baada ya wiki ya pili ya michezo ya kuwania kufuzu CAN 2019, Gabon ina pointi moja na inachukua nafasi ya 3 katika kundi hiyo ambayo Mali inaongoza kwa pointi 6 na timu ya taifa ya nyota  Berahino, Burundi inachukua nafasi ya pili ikiwa na pointi 4.

Mbaya zaidi ya kocha huyu baada ya kushindwa kufanya vizuri dhidi ya Burundi (1-1), Mhispania aipoteza mchezo wake wa kirafiki Juamanne wakiwa Nyumbani tena dhidi ya Zambia (0-1).

Hakuna maoni