MISHE-BOY

Sport | Akiwa na Miaka 51, Rais Weah alcheza mechi dhidi ya Nigeria

Baada ya miaka 15 kuacha kucheza soka, Raisi wa Liberia George Weah alishiriki Jumanne katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria (1-2). Tukio hili limeandaliwa ili kuondoa namba 14 iliyovaliwa na mfungaji wa zamani wa nchi hiyo ambaye kwasasa ni Raisi

Kupata Raisi wa nchi anayeusika na kucheza soka ya kimataifa ni vigumu sana hata hivyo ilitokea Jumanne huko Monrovia. Akiwa kiongozi wa nchi ya Liberia kwa karibu mwaka, Geoge Weah alicheza dakika 79 katika timu ya nchi yake dhidi ya wachezaji nyota waliocheza sana katika Kombe la Dunia mwaka wa 2018 ni pamoja na  Wilfred Ndidi (Leicester), Henry Onyekuru (Galatasaray), Joel Obi (Chievo) na Chidozie Awaziem (Porto) wa nchi ya Nigeria.

Licha ya miaka 51 na uzito wa kutosha, Raisi George Weah alionyesha kwamba alistahili kupewa Mpira wa dhahabu mwaka wa 1995. mechi hii kwa kweli ilikuwa hasa kama sababu ya kumpa heshima Raisi huyo ambaye kwasasa ni  mwanasiasa.

kwenye ardhi ya Liberia, Liberia ilishindwa 2-1 kwa mabao ya Henry Onyekuru (12) na Simeoni Nwankwo (33) pamoja na bao pekee ya Liberia ilipachikwa na Kpah Sherman kwa penalty.

Hakuna maoni