News | Baada ya Big Fizzo ni zamu ya Zehot na Judy kuaga ukapela
Baada ya kiongozi wa Bantou Bwoy Record, Big Fizzo kuaga ukapela siku chache zilizopita hatimaye watangazaji wawili, Rukundo Aboubakar maarufu Zehot wa Classic FM na Ngm257 pamoja na mtangaji mrembo wa Radio La Colombe FM, Gihimbare Judi Caelle wamefunga ndoa Ijumaa Septemba 14, 2018.
Zehot alifunga ndoa leo Ijumaa jijini Bujumbura na kuhudhuriwa na watu wake wa karibu, wa familia yake na familia ya bibi harusi.
Watangazaji hawa waingia katika orodha ya watu maarufu waliofunga ndoa mwaka huu ikiongozwa na nyota wa muziki wa Bujafleva Big Fizzo.
Kwa niaba ya timu nzima ya Tangaza Media Mishe tunawapongeza kwa hatua hii muhimu katika maisha yao
Post a Comment