Sport | Rasmi Fofila PF yapewa taji ya Ubingwa baada ya kuitambia Ubuntu FC
Ligi kuu ya soka ya wanawake nchini Burundi imeingia katika wiki yake ya 13 na tayari klabu ya Fofila PF ya mkoani Ngozi imekuwa rasmi bingwa msimu huu wa 2017-2018.
Klabu ya Fofila PF imeitambiwa timu ya Ubuntu Fc kwa bao nane kwa moja (8-1), kwa ushindi huwo, timu ya mshambuliaji hatari Sakina imetangaziwa ubingwa msimu huu na pointi 37 uku timu pinzani PVB ya Buyenzi ikiridhika nafasi ya pili na pointi 34 pekee.
Matokeo ya wiki ya 13 ya michuano ya ligi ya soka ya wanawake A :
1. Christ Roi 0-1 Lionne Star
2. Rain Bow 0-1 La Colombe
3. PVP Buyenzi 9-0 Onze Étoile
4. Fofila PF 8-1 Ubuntu FC
Msimamo :
1. Fofila PF (Ngozi): 37
2. PVP Buyenzi : 34
3. La Colombe FC : 25
4. Rain Bow (Gitega): 16
5. Lionne Star (Ngozi): 15
6. Ubuntu FC (Kayanza): 13
7. Christ Roi (Gitega): 9
8. Onze Étoile (Kinama): 1
Tuwakumbushe kwamba, Fofila PF kutoka Ngozi ni klabu Bingwa huku timu ya Christ Roi ya Gitega na Onze Etoile ya Kinama zimeshuka daraja na bila shaka zitashiriki ligi ya daraja la pili msimu ujao.
Post a Comment