News | Huyu ndie msanii wa kwanza Afrika Mashariki kukubaliwa kuimba na Fally Ipupa
Msanii wa kizazi kipya wa kike kutoka Burundi mwenye hit mbali mbali kama Shikilia na video yake ya WANGU aliyomshirikisha Shebah wa Uganda, ambayo ilivuka mipaka mpaka vituo vya nje, Natacha a.k.a La Namba-LaBamba-Natacha-Nomaa amekuwa msanii wa kwanza wa kizazi kipya Afrika Mashariki kuwa accepted na management ya nyota wa DR Congo, Fally Ipupa kwa kuimba naye wimbo.
Licha ya Fally Ipupa kutembea nchi za Afrika Mashariki kama Tanzania, Rwanda hakuweza kukubali kufanya collabo na msanii wowote yule hata Diamond Platnum hakukubaliwa.
Kufanya kazi na Fally Ipupa ni moja ya hatua kubwa kwa msanii kutoka Afrika Mashariki, hata mtu akitazama video ambayo inabeba jina DUGA utakuwa na uhakika kuwa ni video ya kimataifa.
Natacha alichukua mda mfupi katika uzinduzi wa Video yake hiyo kwenye ukumbi wa Hotel Club Du Lac Tanganyika kwa kutoa shukran kwa wote waliomsaidia kukamilisha kazi yake hiyo na kusema,
"Nachukua fursa hii kuipongeza management yangu na watu wangu wa karibu kwa kazi nyingine bora na ya kujivunia na vile vile nitumie fursa hii kuwapongeza mashabiki wangu kwa uvumilivu waliokuwa nao na kwa kunionesha ushikamamo wao katika tamasha zangu mikoni pote na mjini kati, mimi ni msanii wa pekee Afrika mashariki kufanikisha kuimba na Fally Ipupa najua wengi walijaribu bila mafanikio ndio maana nitabaki kuwa LA NAMBA".
Post a Comment