Sport | Nyota wa Chibuto FC ajiunga na klabu ya Zambia
Msambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Juhainy Uthuman Cheikh amejiunga na klabu ya Zambia inayoshiriki michuano ya Ligii Kuu ya Zambia kutoka Chibuto FC.
Chibuto Fc ya Mozambique imemuuza Juhainy Uthuman Cheikh kwa klabu ya NAPSA STARS UNITED, akisaini mkataba wa miezi sita (6), klabu imesema katika taarifa yake.
Juhainy Uthuman Cheikh amesema pendekezo ya Napsa United hangeweza kuikataa na amefurahi kuona klabu imekubali ombi lake la kusaini mkataba wa miezi 6 tu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Burundi tayari amekwisha shiriki mechi mbili ya kirafiki na klabu yake mpya, nakufunga bao tatu (3), kwasasa anakua miongoni mwa wachezaji wa Burundi kuelekea Zambia baada ya kiungo wa Messager Ngozi, Enock Nsabumukama na Dieudonne Ntibahezwa walipojiunga na Zesco United.
Post a Comment