MISHE-BOY

Sport | TP Mazembe : Ley Matampi akataa kuongeza mkataba na anaweza kuondoka

Ley Matampi, kipa wa Kimataifa wa DR Kongo, mkataba wake umefika mwisho na hakuongeza kwasasa anajikuta kwenye soko.
''TP Mazembe inatangaza kuwa imekubali ombi la Ley Matampi  kuondoka kwenye klabu mwisho wa mkataba wake ambao  unamalizika Jumamosi, Machi 03, 2018, ''  imeandikwa kwenye tovuti yake rasmi ya TP Mazembe.

Akiwa katika klabu tangu alipofika kutoka AS Vita Club mwaka 2011, Kipa huyo alitumia mkopo wa miaka miwili katika klabu Kabuscorp ya Angola (2013-2015) na mwaka mmoja katika klabu ya DC Motema Pembe (2016) kwa mkopo. kwa hivo, kipa mwenye umri wa miaka 28, Ley Matampi yuko sokoni.

Hakuna maoni