Sport | Kocha Yaoundé aanza kwa kishindo na hizi ndio sifa zake
Kocha mpya wa Vital'o FC, Jean-Gilbert Kanyankore Kagabo al marufu kama Yaoundé, anarudi katika timu ya Vital'o kwa kishindo.
Kocha huyo ameanza kazi yake kama kocha mkuu wa Vitalo hapo jana dhidi ya Flambeau de l'Est ya Ruyigi na kupata ushindi wa kwanza kwa bao moja bila (1-0), bao ilipachikwa na mchezaji Joseph Kashindi katika kipindi cha kwanza.
Kwa mtazamo wa karibu wapenzi wa soka ususan mashabiki wa Vitalo wamefuraia maamzi ya kiongozi wa klabu na kumuona Kocha Yaoundé kuwa anakidhi vigezo vya kuendana na dira ya klabu ambayo ni kukuza na kuwaendeleza wachezaji na kushindana kwa kiwango cha juu kwa lengo la kuwa mabingwa katika mashindano mbalimbali ambayo timu inashiriki.
Uongozi wa Vital'o FC umethibitisha kumpatia ushirikiano wa kutosha ilikufanikisha malengo na mipango thabiti ya klabu.
Sifa kubwa kocha huyu kamwe wapenzi wa soka nchini Burundi hawatosahau ni tarehe ya 01/06/2013 nchini Darfour Vital'o chini ya uongozi wa kocha Jean-Gilbert Kanyankore Kagabo al marufu kama Yaoundé waliibuka washindi wa kombe ya CECAFA Kagame cup kwakuishinda APR ya Rwanda na kuweka rikodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Burundi kutwaha kombe la CECAFA Kagame Cup tangu mwaka 1967, yote kwa mchango mkubwa wa kocha Jean-Gilbert Kanyankore Kagabo.
Post a Comment