MISHE-BOY

Newz | Uzinduzi wa Album ya LIll'p hautofanyika, Vaton Records yawataka radhi


Anaitwa Niyintunze Privato kwa jina halisi, maarufu kama Lill'P, msanii wa Burundi mwenye makazi yake nchini Australia jijini Adelaide ( Southern Australia) amesikika na kujizatiti mbele ya warundi kwa wimbo wake YOU YOU YOU aliomshirikisha Bennie Gunter wa Uganda na FIND YOU aliorikoda chini ya Golden Record kwa Kook K. 

Msanii huyo ndie msanii wapekee aliepo chini ya management ya Vaton Records iliopo nchini Australia. Imefahamika kuwa mwezi May 12 ndipo atakapo weza kuzindua album yake iliopewa jina la Murderweapon na tiketi zilikua zimeshaanza kuuzwa kwenye vituo tofauti nchini humo.

Taarifa tulizonazo ni kuwa uzinduzi huo hautofanyika tena kwa sababu zisizo julikana, 
''Yeah, ni kweli uzinduzi huo tumeuvunja  kwa sababu ambazo zipo juu ya uwezo wetu, lakini mashabiki wetu wasivunjike moyo, tunawapenda na kuwajali, hata kama uzinduzi wa album umesitishwa lakini kuna Tour ya uzinduzi wa video mpya TELL DEM BWOYS tutakayo ifanya Melbourne, brisbane na Perth'', amesema Lill'P

Tulipo taka kujua sababu ni zipi haswa hatukupa nafasi hiyo ila ameongeza  kusema  '' Tunaomba radhi kwa mashabiki  wetu wanguvu waliojitokeza kwa kununua tiketi zao kwa muda maalum, wote watarudishiwa pesa zao ''.


Hakuna maoni