Sport | Kidumu na Mzee Theodore wathibitisha uwepo wao jumamosi hii
Mwanamuziki kongwe pia maarufu Afrika Mashariki kutoka Burundi, Nimbona Jean Pierre maarufu kama Kidumu Kibido alithibitisha uwepo wake kwenye mechi ya kirafiki na ya kuzidisha upendo kati ya wanamuziki wa Burundi Fleva dhidi ya watangazaji wa michezo Burundi (FC Media).
Tofauti na kazi ya muziki mwanamuziki huyu aliwataka mashabiki zake waje kwa wingi kumuona atakavyo wapiga chenga watangazaji na kuwafunga mabao endapo atapata nafasi.
Aidha upande mwingine, mtangazaji maarufu Burundi wa Radio na TV ya taifa mzee Theodore alionesha kufuraishwa sana kwa mechi hiyo na kuwataka wapenzi wa michezo Burundi waje kwa wingi kwenye uwanja wa Mwana Mfalme Prince Louis Rwagasore kushuhudia mechi hiyo ya kuleta amani na furaha kwa mashabiki wa muziki na wa michezo.
Bila shaka itapendeza sana mechi hii kuwaona wazee wawiwili Kidumu na upande mwingine Theodore kila mmoja akionesha kiwango chake.
Hii mechi sio ya kukosa ninaimani ni moja ya kitu kitakacho leta furaha maishani mwetu mwaka hhu wa 2018.
Aidha mechi imepangwa January 13, 2018 saa tatu (9h00) na kiingilio ni pesa miatanu tu (500fbu) kwenye uwanja mkuu Prince Louis Rwagasore.
Post a Comment