MISHE-BOY

Video | Sababu ya warembo Gigy Money na Amber Lulu kuonekana sana na Gaga Blue sehemu zote


Msanii maarufu Burundi, Gaga Blue anayetamba na kibao chake ''Ivo Ivo'' akimshirikisha Yound D kutoka Tanzania, alifunguka kuhusu habari inayoongelewa na mashabiki zake na wengine kuanza kutengeneza habari nyingi tofauti na ukweli.

Gaga Blue alisema kuwa siku hizi anasumbuliwa na maswali mengi na waandishi wa habari wa bongo Fleva uku ni kama wote wakiuliza swali moja na kutaka kujua kilicho kuwa kati yake na mrembo Gigy Money.
Tukumbuke msanii huyu aliwai kuzungumza kwenye Azam Tv na kutamka kauli kwamba
  ''imetokea kwa Dogo Janja kutoka kimapenzi na kuchukua jiko mojakwamoja mrembo Oprah, sio maajabu kwangu yanaweza tokea''.

kauli hiyo inazidi kuleta utata uku wengi wameanza kusema kuwa msanii huyo kutoka Burundi mwenye makazi yake nchini Tanzania, Gaga Blue anatoka kimapenzi na mrembo Gigy Money'.

Aidha msanii Gaga Blue alifunguka na kusema kwamba, " siku hizi sipati usingizi na maswali ya mashabiki pia watangazaji wanao taka kujua ukweli ao usiano wangu na warembo hawo (Gigy Money na Amber Lulu) nafikiri wote wanatambua nimekwisha fanya kazi nawo kwenye video yangu mpya 'Nakupenda' ila ni kweli kila mara naonekana sana nawo ata kwenye vipindi ni kwasababu ni warembo wanao penda kazi zangu pia wanapenda sana kusikia ninavyozungumza kiswahili''. 

Msanii huyu ameendelea na kusema kwamba chochote kile kitakacho tokea na warembo hawo basi itakua imebidi kwasababu wote ni binadamu, alipo ulizwa ni kitu gani aswa kitatokea,  alicheka na kusema '' ni mambo binafsi tu itakapo tokea basi ndio habari ila hakuna kinachoendelea kati yangu na warembo ambao nawapenda sana na wawo wanapenda kazi zangu'', alimalizia Gaga Blue.

tazama Video wakiwa Studio pamoja.

Hakuna maoni