Golf | Kijana mdogo mwenye kipaji kwenye mchezo wa Golf Burundi
Anaitwa Habib Suleimani mchezaji wa Golf Burundi mwenye umri wa miaka 13, ameanza kucheza mchezo wa Golf 2011.
Baada ya kuonesha kipaji chake na kupendezwa na kocha wake, licha ya umri wake mdogo amezidi kushangaza wengi na kuingi katika Kipengele (Categori) cha pili na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa golf mdogo 2014.
Kitu kilicho mtuma Kijana huyu kucheza mchezo wa golf wakati ni mchezo unafahamika kama mchezo wa matajiri, Habib alisema kuwa ni mchezo wakutulia na ndio moja ya sababu ya yeye kuupenda mchezo wa golf.
Habib alifunguka zaidi kwakuchaguliwa kijana mdogo pekee katika timu ya taifa Burundi,
'' Ninafuraha sana kuona nazidi kutimiza ndoto zangu na hii ni moja ya hatua kubwa nazidi kufikia. Nitapendelea kuendelea.''
Aidha habib alimtaja mchezaji wa golf anaependa duniani na ana ndoto ya kucheza naye pia aliomba ombi kwa viongozi wa serikali kuikumbuka mchezo wa golf,
''napenda kucheza na Rory pia ningependa kucukua fursa hii kuwaomba sana viongozi ambao tunafahamu sana ni matajiri pamoja na raisi wa nchi, wakumbuke kuwa kwenye michezo sio mchezo wa mpira tu na golf pia, ni mchezo ya matajiri ila tuna matajiri wengi Burundi hawachezi gofl mpaka sasa sijaelewa kwanini''. Alisema habib Suleiman
Post a Comment