Officiel | Kara Mbodji aondoka Nantes baada ya kupigana na Kocha wake
Beki wa kimataifa wa Senegal na Nantes FC, Kara Mbodji aliachana na timu yake na kjiunga na Anderlech baada ya kupigana na kocha wake.
Baada ya kufanya miezi sita, Kara Mbodji mwenye umri wa miaka 29 aliamua kuondoka ili awe mbali na kocha Vahid Halilhodzic baada ya kukosa maelewano kati yao wawili.
Kocha Vahid Halilhodzic, anaonekani ni mubishi sana kwa mjibu wa Mbodji, ndio sababu ya beki huyo kuamua kurudi Anderlecht.
Timu ya Anderlecht ilithibitisha Ijumaa usiku kurudi kwa beki huyo wa Senegal, akiwa chini ya mkataba hadi Juni 2020.
Kisa cha ugomvi wake na kocha Vahid Halilhodzic, kara analalamika kwanini apewi nafasi msimu huu na mbaya zaidi katika mechi Jumanne ya Ligue 1 dhidi ya MontPellier (2-0 kwa ushindi wa Nantes), Mbodji hakuridhishwa kwa kitendo cha kuondolewa dakika la 60 na kukataa kumsalimu kocha wake Vahid Halilhodzic.
Bifu iliendelea mpaka kwenye mu vestiaire na kufikia hata kushikana huku wachezaji wakiingilia kati.
Tangu alipofika nchini Ufaransa Julai mwaka jana, Mbodji alicheza michezo 6 tu ya ligi na moja ya kombe la Ufaransa (Coupe de France) na moja Kombe ya ligi ( Coupe de la ligue)
Post a Comment