MISHE-BOY

Sport | Saidi Ntibazonkiza arejea nyumbani baada ya miaka kadhaa

Aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa Intamba Murugamba, Saido Ntibazonkiza arejea nyumbani baada ya kuwa nje ya nchi ki soka kwa miaka kadhaa.

Licha ya kufanya vizuri katika Ligi mbali mbali za Ulaya hakuwa anaitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa Burundi. 
Ujio wake tayari wengi wameanza kuzua mambo mengi na kusema kwamba kuna  uwezekano wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 akarejea katika timu ya taifa kwa mara nyingine tena ili kuongeza chachu kwa taifa ilo ambalo litakua na michezo miwili ya kuwania kushiriki Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Mali.

Habari tulizo zinasa hivi karibuni ni kwamba, Ntibazonkiza yuko mjini Bujumbura  kwa mapumziko zaidi na kuiangalia familia yake huku hakuna mwaliko wowote wa timu ya taifa kwa sababu kocha mkuu wa timu ya taifa Intamba Murugamba, Olivier Niyungeko hajaweka wazi orodha ya wachezaji watakao jiandaa  kwa mchezo wa Oktaba 12 nchini Mali  na 16 mjini Bujumbura.

Hakuna maoni