News | Watangazaji wa 5 wa Buja FM wasimamishwa
Kituo cha Radio Buja FM nchini Burundi kilisimamisha kazi watangazaji wa Habari wake wa 5 wanao tangaza habari za michezo.
Mkurugenzi wa Radio Buja FM, Franck Tumwekase ameitisha mkutano wa waandishi wa habari kutoka vituo tofauti ambapo alitaka kuweka wazi kuhusu mgogoro kati ya waandishi wa habari waliosimamishwa.
Mbele ya waandishi wa habari kadhaa, mkurugenzi wa Buja FM alifafanua kuwa kamwe hawezi kuvumilia aina yoyote ya tabia mbaya katika kituo yake.
Watangazaji wa habari 5 wa kituo hicho wamesimamishwa kazi kwa miezi 2, ni pamoja na Alain Muhirwe, Elvis Iradukunda, Kevin Gakiza, Landry Rukundo na Arsene Bucuti, wote wakiwa watangazaji wa michezo katika kipindi maarufu nchini "B Sport".
Kulingana na kauli ya Mkurungezi wa Buja FM, Franck amesema kwamba tabia mbaya imeanza kuonekana kipindi walianza kutangaza Kombe la Dunia kwenye ma baa, na ilihitajika uhamisho ili watangazaji waendelee kutangaza habari kwenye ma baa. Wakati kampeni ilikuwa imekwama, waandishi wa habari hawa walimwambia kuwa hawatakuja mahali pa kazi, ishara hii haikumfuraisha Mkurugenzi ikasababisha na ukweli kwamba usimamizi uliamua kuwapa gharama za ziada kwa watangazaji wa habari waliobaki kituoni katika kipindi cha kampeni hii.
Kwa sura hii, haiwezekani mtangazaji wa habati aharibu kazi yake bila sababu sahihi, usimamizi wa radio hiyo iliwasimamisha watangazaji hawo kwa swali la Uchunguzi zaidi.
"kwa wale wanaofikiri ninaweka maslahi binafsi ndani yake, sijaficha chochote nilicho kitumia nimesoma sheria, kumbukeni sijaanza mimi kuwasimamisha ila wao ndio ambao waliacha kazi. alisema Franck Tumwekase.
Kulingana na kauli ya Franck Tumwekase, watangazaji watano waliosimamishwa walidai ongezeko la bahasha ikilinganishwa na kampeni ya kutangaza kombe la dunia hii ya 2018.
"'watu watambuwe kwamba kuliko kutangaza mechi hizi, walikuwa wakifanya kazi zao. sasa tutaanza uchunguzi, lakini wakati huo huo wamesimamishwa. Ukosefu wa adabu hauna nafasi katika redio yetu ata siku moja". Alimalizia Franck.
Post a Comment