MISHE-BOY

Sport | Imboneza FC ya New Generation yarudi Burundi na Kombe

Timu ya soka ya watoto wa Mitaani ya Burundi inayofahamika kwajina la Imboneza FC ikidhaminiwa na New Generation Burundi ambayo inazidi kupambana na uwepo wa watoto katika hali za barabara kwasasa ina watoto zaidi ya 600 kwenye safu zake.

Imboneza FC ilirudi nchini Mei 19, 2018 ikitoka katika mashindano ya Kombe la Dunia ya watoto wa mitaani mjini  Moscou, Kombe la Dunia la soka inayofanyika miaka baada ya  miaka.

Mwaka huu, michuano ilianza Mei 11 katika mji wa Moscow nchini Urusi, timu 24 za wasichana na wavulana wanaowakilisha nchi 21 huku Bara la Afrika ikiwakilishwa na  nchi tatu ambazo zimechaguliwa kushiriki Kombe hilo ni pamoja na Kenya, Liberia na Burundi pia timu moja ya wasichana  kutoka Tanzania.

Kwenye michuano hii nchi ya Burundi iliwakilishwa na timu Imboneza FC  ya shirika la New Generation kinachoongozwa na mzee Dieudonné Nahimana.

Katika michezo miwili ya kwanza timu ya Imboneza FC ilishinda Indonesia  na Brazil (2-0 na 4-1) kwa ushindi huwo iliwapa fursa ya kufikia robo fainali na kukabiliana na Belarus huku bila shaka Imboneza FC iliitambia timu ya Belarusi kwa kuichapa bao mbili bila (2-0).

 Katika mechi ya nusu fainali, timu ya Imboneza FC imepoteza mchezo dhidi ya Uzbékistan (0-1), kwa hiyo warundi hawo walipata fursa ya kucheza fainali ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Indonesia na kuibuka mshindi kwa bao tatu kwa moja (3-1).

Kwa hiyo Imboneza FC ilirudi nchini ikishikilia Kombe huku nahodha wa timu, Asman Bigirimana alimaliza mashindano hiyo na bao 5 akiwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia (Street Child World Cup 2018)
Nahodha wa  timu Bigirimana Asman alisema : Nimevutiwa sana na michuano hiyi, maadili binafsi ya kila mtu ilionekana kwenye safari na sisi wote tulikua tunahitaji ushindi mpaka kuchukua nafasi ya kwanza, pamoja na kushindwa ila tulikuwa na fursa ya kufika mpaka fainali. naweza kusema kuwa mwaka huu tulikua bora zaidi kuliko mwaka 2014 na kila timu ilijiandaa vilivyo kutafuta mbinu ya kutushinda.

Niwakumbushe pia haya mashindano yaliyoandaliwa nchini Urusi ili kujiandaa kwa Kombe la Dunia 2018 ambayo itaanza rasmi nchini hapo kuanzia Juni 14 hadi Julai 15,2018.

Hakuna maoni