MISHE-BOY

Sport |Moussa Omar kujiunga na Sofapaka FC

Mchezaji wa timu ya taifa Intamba Murugamba wa Bugesera FC ya Rwanda, Moussa Omar maarufu kama Moussa Dejong amekamilisha uhamisho wake kuelekea Sofapaka baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya CECAFA2017 nchini Kenya.

Kwenye ukurasa wa Facebook, klabu ya Sofapaka wameripoti kufanikiwa kunasa saini ya kwanza katika dirisha hili dogo la usajili beki kutoka Burundi kutoka klabu Bugesera ya Rwanda.
Aidha Sofapaka wameripoti kutumia dola Elfu 15 (15.000$)  kumsajili Moussa Omar.

Hakuna maoni