Sport | Kocha wa Golf Junior Academic aeleza sababu ya kudorora kwa mchezo wa Golf nchini Burundi
Kocha mkuu wa Golf Junior Academic nchini Burundi, Kudra Nahimana aendelea kuandaa wachezaji wake kwa mashindano itakayo zinduliwa hivi karibuni nchini Kenya.
Mkufunzi huyu amemendelea na kuwataka waeshimiwa kama Gervais Rufyikir ata raisi Mzee Peter Nkurunziza na viongozi wote ambao wanauwezo waje kucheza mchezo wa Golf kwasababu ni mchezo unayojulikana kama mchezo wa watajiri ila hakuna ata tajiri moja wa Burundi anaecheza mchezo huwo kinyume na Muhamed Rukara.
Aidha kocha huyu ameendelea kusema kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia kudorora kwa mchezo huwo ni kuvamiwa na mamluki wasiokuwa na dira wala mwelekeo wa kuendeleza na yote ni kwasababu viongozi na matajiri wamezamia kwenye mchezo wa soka tu.
Kocha huyu alifungukia Mishe Mishe na kusema ''Tunapaswa kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kunusuru mchezo wa Gofl wa Burundi kwasababu nina vijana wengi wanavipaji na wanaitaji msaada mkubwa kwa kuiwakilisha Burundi Kimataifa zaidi, tusaidiane kwa kunusuru mchezo huu kutoka mikononi mwa watu wanaoitwa 'wasaka tonge'. '' Alisema Kocha Kudra Nahimana
Post a Comment